Thursday 25 June 2015

NEW MUSIC:FunCulture Ft Lecture-Nogesha.


Msanii chipukizi FunCulture ameachia rasmi ngoma yake mpya inayoitwa Nogesha aliyomshirikisha Lecture iliyofanyika katika studio ya Kamosage Records chini ya Producer G-Touchez.

FunCulture:Naamini Ujio Wangu Wa Sasa Ni Wa Kishindo.


FunCulture

Msanii Chipukizi kutoka Mkoa wa Geita FunCulture amesema.."kwa sasa anaamini ujio wake utakuwa wa tishio na wa kipekee katika muziki..ngoma ipo tayari na leo hii hii itakuwa released''....Alisema hayo baada ya kukamilisha track yake mpya inayokwenda kwa jina la Nogesha akiwa kamshirikisha Lecture chini ya Producer G-Touchez katika studio ya Kamosage Records iliyopo mkoani Geita.

FAHAMU KUHUSU MWANAMUZIKI BRUNO MARS:

Bruno Mars, Las Vegas 2010.jpg
Bruno Mars


Peter Gene Hernandez (amezaliwa 8 Oktoba 1985), kitaaluma anajulikana kwa jina lake la kisanii Bruno Mars, ni mwimbaji, mtunzi, mtayarishaji wa rekodi, mwigizaji sauti, na choreographer. Alizaliwa na kukulia katika Honolulu, Hawaii na familia ya wanamuziki, Mars alianza kufanya muziki katika umri mdogo na kutumbuiza katika kumbi mbalimbali vya muziki katika mji wake katika utoto wake. Alipomaliza shule ya sekondari na kuhamia Los Angeles kufanya mambo yake ya muziki. 

Alishawahi kufanya kazi  na Motown Records,baada ya hapo alisaini na Atlantic mwaka 2009. Alijulikana kama mwanamuziki wa kujitegemea baada ya kuto wimbo wake wa "Nothin On You" akiwa na Bob, na "Billionaire"akiwa  na Travie McCoy, ambayo ilikuwa na Mafanikio duniani kote. Studio yake albamu, Doo-Wops & Wahuni (2010), ilimtambulisha Marekani Billboard Hot 100 chati-topping single "The Way You Are" na "Grenade", na n "Lazy Song ". Albamu yake ya pili, unorthodox Jukebox, ilitolewa mwaka 2012, ilipata kushika nafasi namba moja nchini Marekani,zikiwemo nyimbo "Locked Out Of Heaven", "When I Was Your Man" na "Tressure".
s
s
s
Mars amepokea tuzo nyingi na uteuzi, zikiwa mbili za Grammy na alitajwa moja ya watu 100 katika gazeti la Time Magazine kwa umaarufu katika ulimwengu, mwaka 2011. Katika mwaka 2014, yeye alikuwa "Msanii wa Mwaka" katika Billboard na nafasi namba moja katika Forbes 30. Kupitia kazi yake ya kuimba, ameshauza zaidi ya albamu milioni 12 na single milioni 68 , na hivyo kumfanya kuwa  msanii mwenye mauzo mengi zaidi ya kazi zake duniani.Hata hivyo, kama mtumbuizaji, mwandishi na mtayarishaji mauzo yake jumla yalivuka single milioni 130 .Katika mauzo yake single zake tano zilionekana kuwa miongoni single zilizouza zaidi duniani. Mars sasa mwanamuziki mwenye mafanikio zaidi duniani.

Wednesday 24 June 2015

WAFAHAMU MASTAA WATATU WALIOZALIWA SIKU YA LEO






Solange Knowles
WAFAHAMU MASTAA WATATU WALIOZALIWA SIKU YA LEO
Ni muimbaji,model pia ni mdogo wa Beyonce Knowles.Alitoa album yake ya kwanza iliyoitwa  Sol-Angle and hardley St Dreams ambayo ilishika nafasi ya 9 katika chati za Bilboard 200.
Alianza kufanya baby jams na hip hop toys kabla hata hajaanza kusoma.Aliolewa na Daniel Smith mwaka 2004 na kupata mtoto mmoja waka huohuo aliyeitwa Daniel Jr,mwaka 2007 walitengana na mumewe huyo na kuolewa tena mwaka 2014 nam Alan Ferguson.Solange ni Mtoto wa Matthew na Tina Knowles.Alizaliwa June 24 mwaka 1986 huko Texaz,ana miaka 29.

Lionel Messi
Nyota mshambuliaji wa mpira Lionel Messi anayechezea FC Barcelona Pia ni Captain wa Timu ya Taifa ya Argentina.Alizaliwa June 24 mwaka 1987 huko Argentina,ana miaka 28.

Mindy Kaling
Ni muigizaji nyota aliyecheza filamu ya No String Attached mwaka 2011,alizaliwa June 24 1979 Massachusetts,Ana miaka 36.

MTUNZI WA WIMBO "MY HEART WILL GO ON" AFARIKI DUNIA.

Mtunzi wa nyimbo wa Hollywood,James Horner.aliyeandika wimbo wa My Heart Will Go On uliotumika katika filamu ya Titanic,amefariki kwenye ajali ya ndege yake binafsi.
Ndege yake ilianguka katika msitu wa mbuga ya Los Padres National Forest,kaskazini mwa Los Angeles.Horner alikuwa mwenyewe kwenye ndege hiyo.
Celine Dion,aliyeimba wimbi huo uliompa Horner tuzo za Oscar alituma salamu za rambi rambi kwenye Twitter:Shaken by tragic death of James Horner.We send our prayers and deepest condolences to his family and friends."Alitweet.James Horner Amefariki akiwa na umri wa miaka 61.

Tuesday 23 June 2015

Albino Killings(KiverT)

Rapper KiverT ambaye pia ni mwanaharakati katika swala zima la haki za binadamu na kuzuia ubaguzi ameonyesha kupinga vikali suala la mauaji ya Watu wenye ulemavu wa ngozi(Albino)kupitia wimbo wake Mpya unaokwenda kwa jina la Inatosha katika wimbo huo KiverT amewahamisishi watu wa jamii zote kupinga mauaji hayo ya kikatili..."Muziki unaplay part kubwa katika maisha ya binadamu na ndio maana nikaamua kuandika wimbo huu ili kuwakumbusha binadamu wote kuwa sisi wote ni sawa na haipendezi kuamini kuwa kumuua mtu mwenye ulemavu wa ngozi itakupa faida yoyote...hivyo basi tuzuie mauaji ya Albino na tuishi kwa usawa"Alisema Kiver,ngoma ya Inatosha tayari ipo katika mitandao mbali mbali akiwa amemshirikisha Lecture Producer akiwa ni G-Touchez!!

KiverT Tz