Tuesday 23 June 2015

Albino Killings(KiverT)

Rapper KiverT ambaye pia ni mwanaharakati katika swala zima la haki za binadamu na kuzuia ubaguzi ameonyesha kupinga vikali suala la mauaji ya Watu wenye ulemavu wa ngozi(Albino)kupitia wimbo wake Mpya unaokwenda kwa jina la Inatosha katika wimbo huo KiverT amewahamisishi watu wa jamii zote kupinga mauaji hayo ya kikatili..."Muziki unaplay part kubwa katika maisha ya binadamu na ndio maana nikaamua kuandika wimbo huu ili kuwakumbusha binadamu wote kuwa sisi wote ni sawa na haipendezi kuamini kuwa kumuua mtu mwenye ulemavu wa ngozi itakupa faida yoyote...hivyo basi tuzuie mauaji ya Albino na tuishi kwa usawa"Alisema Kiver,ngoma ya Inatosha tayari ipo katika mitandao mbali mbali akiwa amemshirikisha Lecture Producer akiwa ni G-Touchez!!

KiverT Tz

No comments:

Post a Comment