Wednesday 24 June 2015

MTUNZI WA WIMBO "MY HEART WILL GO ON" AFARIKI DUNIA.

Mtunzi wa nyimbo wa Hollywood,James Horner.aliyeandika wimbo wa My Heart Will Go On uliotumika katika filamu ya Titanic,amefariki kwenye ajali ya ndege yake binafsi.
Ndege yake ilianguka katika msitu wa mbuga ya Los Padres National Forest,kaskazini mwa Los Angeles.Horner alikuwa mwenyewe kwenye ndege hiyo.
Celine Dion,aliyeimba wimbi huo uliompa Horner tuzo za Oscar alituma salamu za rambi rambi kwenye Twitter:Shaken by tragic death of James Horner.We send our prayers and deepest condolences to his family and friends."Alitweet.James Horner Amefariki akiwa na umri wa miaka 61.

No comments:

Post a Comment